| Mtoto ( kulia ) wa aliyelelewa na mbwa. |
Akizungumza kwa niaba ya mtoto huyo nyumbani kwao, Nyerere B, Mabatini Mwanza, dada wa mtoto huyo, Recho Rojason (18) alisema kuwa mdogo wake bado anateseka kwani hapati malezi ya kutosha kutokana na maisha yao kuwa magumu.
| Baba wa mtoto. |
Recho alisema kuwa, maisha yao yamekuwa magumu baada ya mama yake
kuwatelekeza na kuolewa na mwanaume mwingine huku akimwacha baba yao
ambaye ametopea kwenye ulevi na kushindwa kutoa msaada wowote.
Recho ambaye ni hausigeli anayefanya kazi kwa ujira mdogo maeneo ya Mwanza Mjini, alisema wamekuwa wakipata fedha kidogo kutoka Halmashauri ya Jiji ambapo hazikidhi mahitaji yao na kuwaomba watu wajitokeze kuwasaidia.
Nyumba anayoishi mtoto huyo.
Akizungumzia sakata hilo jirani anayeishi na watoto hao, Chausiku Ibra alisema kuwa watoto wa familia hiyo wamegeuka machokoraa kutokana na huduma hafifu na kuongeza kuwa mtoto wa mwisho (Kulendya) ndiye yupo hatarini zaidi.
“Huyu mtoto wa mwisho ndiye aliye hatarini zaidi kwa kuwa tangu alivyokuwa mtoto alikuwa akiletewa chakula na kutunzwa na mbwa.
Mpaka anakuwa hivi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli. Watoto hawa wanahitaji msaada jamani,” alisema jirani huyo.
Waandishi wetu walijionea, nyumba wanayoishi watoto hao ambayo imeonekana kuharibika kwa kiasi kikubwa sehemu za paa na kuta jambo ambalo ni hatari kwa watoto hao huku taarifa zikieleza kuwa, baba wa watoto hao, Rojason Ernest amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiuguza nyonga baada ya kuanguka akiwa anatokea kilabuni.
Kama umeguswa na unataka kuwasaidia watoto hao, wasiliana nao kwa namba ya jirani yao, Chausiku: 0767445683
Source: GPL
No comments:
Post a Comment